SALAMU

SYNOPSIS:

Ni kisa kinachowahusu watoto wanaotumikishwa Mitaani na Jamii kwa lengo la hiyo Jamii kujipatia Kipato na kuongeza uchumi kupitia watoto hao na bila kujali haki ya Mtoto. Watoto hawa wawili, KAKI (13) na LUNYA (14) walikua wenyeji wa Kigoma Vijijini, Kutokana na Uyatima wao wanaamua kufunga safari na kwenda Dar es salaam ili kutafuta unafuu wa Maisha. Vijana hawa wanapofika Dar es salaam, Wanafikia mikononi mwa MZEE MATEO 54, Mzee mwenye Uchu wa maisha mazuri na kujikuta anaanza kuwatumikisha watoto hawa kwenye biashara ya kuuza karanga mitaani huku Faida yote ni ya kwake na kuwalipa watoto hawa Ujira mdogo. Mzee Mateo anapata ushauri mwingine kutoka kwa ndugu yake wa muda mrefu, kuwa wanaweza kuwatumia watoto hawa kama sehemu ya kuingizia Kipato kingi zaidi hasa kwenye shughuli za wizi wa mifugo na Mazao huko vijijini. Mzee huyu anaona hili ni wazo bora zaidi na kulitendea kazi. KAKI na mwenzie wanaanza kutumika katika shughuli za wizi na kuleta faida kubwa kwa Mateo lakini ujira bado ulikua mdogo pale pale. Kaki na mwezie wanachoka maisha haya na kuanza kutafuta mbinu ya wao kuiona faida Yao kutoka kwa Mateo.

Year: 2019     Duration: 90 min     Language: English, Swahili

WATCH LATER

COMMENTS

SIMILAR FILMS

Top